Mkahawa mwengine washambuliwa Mogadishu

Imebadilishwa: 3 Novemba, 2012 - Saa 13:51 GMT

Watu kama wane wameuwawa na wengine 10 kujeruhiwa katika shambulio dhidi ya mkahawa mjini Mogadishu, Somalia.

Polisi wa Somalia wakisaidia jeruhi katika shambulio la Septemba

Mwandishi wa BBC mjini humo anasema kumetokea miripuko miwili mikubwa nje ya mkahawa huo uitwao "The Village", katika mtaa wa Hodan, kati-kati ya mji.

Walioshuhudia tukio hilo wanasema mabomu yaliripuliwa na watu waliojitolea mhanga.

Mwezi wa Septemba watu 14 walikufa kwenye shambulio katika mkahawa mwengine mjini Mogadishu wa tajiri huyo-huyo.

Mwandishi wa BBC anakumbusha kuwa mashambulio kama hayo hufanywa mara kwa mara, na baadhi yao ni vitendo vya kundi la wapiganaji wa Kiislamu, al-Shabaab, ambao bado wanadhibiti sehemu kubwa ya nchi.

Mashambulio mengine hufanywa na magengi ya wahalifu na wanamgambo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.