Baraza la mawaziri lateuliwa Somalia

Imebadilishwa: 4 Novemba, 2012 - Saa 17:08 GMT

Waziri Mkuu wa Somalia, Abdi Farah Shirdon, ametangaza baraza lake la mawaziri ambalo kwa mara ya kwanza litakuwa na waziri wa mashauri ya nchi za nje mwanamke - Fauzia Yusuf Haji Adan.

Rais wa Somalia

Baraza hilo ni dogo sana likilinganishwa na yale yaliyopita, na litakuwa na mawaziri 10 tu.

Waandishi wa habari wanasema koo nyengine zinaona hazikupata wizara, na huenda ikawa shida kwa bunge kulikubali baraza hilo la mawaziri.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.