Mwanamke wa kwanza waziri wa Somalia

Imebadilishwa: 5 Novemba, 2012 - Saa 15:06 GMT

Fauzia Yusuf Haji Adan

Somalia inatarajiwa kupata waziri wake wa kwanza mwanamke pinde baraza la mawaziri lililopendekezwa na waziri mkuu Abdi Farah Shirdon litakapoidhinishwa na bunge.

Fauzia Yusuf Haji Adan ni mmoja wa wanasiasa kumi waliteuliwa katika baraza la mawaziri ambalo ni ndogo sana na ameteuliwa kama waziri wa mambo ya nje.

Alitaja kuteuliwa kwake kama jambo la kihistoria kwa nchi hiyo na kwa wanawake wa Somalia. Bi Fauzia pia ni naibu waziri mkuu wa Somalia.

Hata hivyo wadadisi wanasema kuwa bwana Shirdon huenda akakabiliwa na kibarua kutafuta kupitishwa kwa baraza hilo na kuna hofu kuwa koo zote huenda zisiwakilishwe kikamilifu.

Bwana Shirdon, ambaye ni mfanyabiashara alichukua wadhifa wake baada ya kuteuliwa na Rais Hassan Sheikh Mohamud na hata kukubaliwa na bunge.

Uchaguzi wa bwana Mohamud mwezi Sepetemba alionekana kuwa Rais wa kwanza wa Somalia kuchaguliwa kidemokrasa kwa miaka 42.

Mawaziri hao wanachukua uongzi wa nchi ambayo haijakuwa na uongozi thabiti kwa zaidi ya miaka 20 huku wababe wa kivita kutoka koo mbali mbali, wapiganaji wa kiisilamu na nchi jirani za Somalia wote wakipigania udbibiti wa Somalia baada ya kupindulia kwa aliyekuwa rais Siad Barre mwaka 1991.

Changamoto kubwa

"Baada ya majidiliano ya muda mrefu na kushauriana , nimeteua baraza la mawaziri, ambalo linajumuisha mawaziri kumi. Miongoni mwao ni waziri wa kwanza mwanamke kwa mara ya kwanza katika historia ya Somalia’’ alisema waziri mkuu.

Bi Adan anatoka katika jimbo la Somaliland lililojitenga na ameishi nchini uingereza kwa miaka mingi.

"Uteuzi wangu kama waziri wa mambo ya nje ni jambo la kihistoria kwa Somalia na hasa kwa wanawake , inafungua ukurasa mpya wa siasa za nchini humo na tutafanikiwa katika uongzi wetu.’’ Alisema bi Adan

Changamoto kubwa inayokabili serikali mpya inayoungwa mkono na Umoja wa matifa, ni wapiganaji wa Al shabaab.

Licha ya kupoteza baadhi ya miji mikuu, wanamgambo hao wangali wanadhibiti sehemu kubwa za kusini mwa Somali pamoja na maeneo ya kati.

Al-Shabab wamefanya mashambulizi kadhaa ya kujitoa mhanga mjini Mogadishu tangu kufurushwa kwao kutoka Mogadishu na majeshi ya Muungano wa Afrika mwaka jana ikiwemo mashambulizi kadhaa baada ya uchaguzi wa Rais Mohamud.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.