Kizungumkuti cha bajeti ya Ulaya

Imebadilishwa: 7 Novemba, 2012 - Saa 10:23 GMT

Angela Markel akizungumza na mwenzake wa Ufaransa Francois Hollande

Chansela wa Ujerumani Angela Merkel anatarajiwa kwenda mjini London, nchini Uingereza hii leo kujaribu kutafuta maafikiano kuhusu bajeti ya matumizi ya Umoja wa Ulaya kuanzia mwaka 2014.

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron ameashiria kuwa anataka bajeti hiyo iwe ya kiwango fulani na anakabiliwa na shinikizo kutoka kwa baadhi ya wanachama wake kukataa makubaliano ya aina nyingine yoyote.

Serikali ya Ujerumani imeashiria kuwa huenda ikakubaliana na matakwa ya Uingereza ya kuwepo udhibiti mkali wa matumizi lakini inaona kuwa kunapaswa kuwa na ongezeko fualani, lakini sio ongezeko ambalo mataifa yaliyo katika eneo la Meditarenia na Mashariki mwa Ulaya yanayotaka.

Huku msimamo mkali wa Uingereza ukizuka, Kansela Merkel wiki iliyopita alisema kuwa tishio la kupinga pendekezo hilo halisaidii.

Ziara yake mjini London inajiri huku baadhi ya wanachama katika chama chake wakionyesha kuchoshwa na kile wanachokiona kuwa ni ukaidi wa Uingereza.

Matamshi ambayo baadhi ya wabunge wa serikali ya Ujerumani wametumia kuiambia BBC kuhusu hali iliyopo ni kuwa Uingereza inapaswa kuamua iwapo inakubaliana nao au la.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.