Rais Omar Al Bashir afanyiwa upasuaji

Imebadilishwa: 7 Novemba, 2012 - Saa 13:04 GMT

Rais Omar Al Bashir

Rais wa Sudan Omar Al Bashir yuko bukheri wa afya baada ya kufanyiwa upasuaji nchini Saudi Arabia.

Duru za serikali zinasema kuwa Rais Bashir mwenye umri wa miaka 68, alifanyiwa upasuaji mdogo katika koo yake mjini Riyadh siku ya Jumanne.

Taarifa za upasuaji huo zilitokea siku moja baada ya kuripotiwa kuwa bwana Bashir angefanyiwa ukaguzi wa kimatibabu kabla ya kukutana na mfalme wa nchi hiyo.

Mwezi jana maafisa walisema kuwa Bashir alifanyiwa upasuaji mjini Qatar.

Mnamo Jumatatu, idara ya shirika la habari la serikali Suna, nalo lilisema kuwa Bashir alikwenda Saudia kwa ukaguzi mdogo tu wa kimatibabu kuhusiana na koo yake vile vile.

Inasemekana Rais Bashir amepona na anaendelea na majukumu yake kama kawaida. Bwana Bashir anatakikana na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita kufuatia madai kuwa alikiuka haki za binadamu katika jimbo la Darfur, madai anayoyakana.

Amekuwa mamlakani nchini Sudan tangu mapinduzi ya kijeshi yalifofanyika mwaka 1989.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.