Kiongozi wa zamani libya kizimbani

Imebadilishwa: 8 Novemba, 2012 - Saa 09:14 GMT

Mustafa Abdul Jalil

Mahakama nchini Libya imeamuru kuhojiwa kwa kiongozi wa zamani wa mpito Mustafa Abdul Jalil kuhusiana na mauaji ya kamanda mkuu wa zamani wa waasi Abdel Fattah Younes mwaka jana.

Bwana Jalil, aliyekuwa mwenyekiti wa lililokuwa baraza la mpito,wakati jenerali Younes alipigwa risasi, alitoa maelezo tatanishi kuhusu mauaji yake.

Watu kumi na moja wameshtakiwa kuhusiana na kesi hiyo.

Generali Younes alishukiwa sana kwa sababu ya uhusiano wake wa karibu na hayati Muamar Gaddafi.

Kamanda huyo alikuwa mmoja wa kundi la watu waliosaidia Gaddafi kuingia mamlakani mwaka 1969. Alihudumu kama waziri wa mambo ya ndani kabla ya kupanda ngazi na kuwa afisaa mkuu jeshini kujiunga na waasi mwezi Februari mwaka jana.

Miezi kadhaa baadaye, mwili wake ulipatikana viungani mwa mji wa Benghazi ukiwa na alama za risasi.

Mauaji yake yalifanyika muda mfupi baada ya kibali cha kukamatwa kwa Generali Younes kutolewa ili aweze kuhojiwa.

Taarifa mbali mbali kuhusu alivyouawa kamanda huyo zilitolewa na maafisa wakati huo ikiwemo bwana Jalil.

Mwanawe bwana Younes aliyehudhuria kusikizwa kwa kesi hiyo alisema uamuzi wa mahakama ulikuwa hatua nzuri sana.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.