Shule na makanisa zateketezwa Nigeria

Imebadilishwa: 9 Novemba, 2012 - Saa 14:17 GMT

Shambulizi dhidi ya kanisa

Jeshi la Nigeria linasema kuwa polisi watatu wameuawa katika mashambulizi yaliyofanyika usiku kucha dhidi ya kituo cha polisi Kaskazaini Mashariki mwa nchi.

Msemaji wa polisi alielezea kuwa makanisa matatu pamoja na shule moja ya msingi ziliteketezwa wakati wa shambulizi hilo mjini Buni Yadi katika jimbo la Yobe.

Aliongeza kuwa wavamizi waliiba silaha kutoka kwa kituo hicho cha polisi.

Haijulikani nani aliyefanya shambulizi hilo ingawa kundi la Boko Haram limekuwa likifanya mashambulizi ya mara kwa mara Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.