Mkurugenzi Mkuu wa BBC ajiuzulu

Imebadilishwa: 10 Novemba, 2012 - Saa 21:38 GMT

Mkurugenzi mkuu wa shirika la BBC, George Entwistle, amejiuzulu.

George Entwistle ajiuzulu kama Mkurugenzi BBC

Amekuwa akishutumiwa kwa namna alivyoshughulikia taarifa iliyopeperushwa katika kipindi cha Newsnight.

Taarifa hiyo kwa makosa ilimshutumu aliyekuwa Waziri wa Fedha wakati wa serikali ya Conservative , Lord McAlpine, kwamba alihusika katika kashfa ya kudhalilisha watoto.

Tayari shirika la BBC limekuwa likichunguzwa vikali katika kashfa inayomhusu mtangazaji wake wa zamani Jimmy Savile kwa madai ya kuwadhalilisha watoto.

Kipindi hicho cha Newsnight kinadaiwa kuacha kwa makusudi kutangaza habari ya uchnguzi kuhusiana na kashfa ya Bwana Savile.

Wakati wa kutangaza kujiuzulu Jumamosi,usiku Bwana Entwistle alisema "ilikuwa ndilo jambo la heshima kwangu kulifanya".

Akisimama kando yake Mwenyekiti wa BBC Trust, Lord Patten alisema " huu ulikuwa moja wapo ya usiku wa majozi katika maisha yangu ya umma".

"Muhimu kwa BBC ni jukumu lake kama chombo cha habari kinachoaminika"

"Kama Mhariri Mkuu wa shirika hili la habari, kwa heshima kubwa George amehiari kujiuzulu kutokana na makosa yasiokubalika - uanahabari mbovu ambayo umezua malalamiko mengi".

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.