Wachimba migodi bado wagoma

Imebadilishwa: 10 Novemba, 2012 - Saa 16:35 GMT

Maelfu ya wachimba migodi wa Afrika Kusini wamekataa kurejea kazini, katika kampuni ya dhahabu nyeupe kubwa kabisa duniani iitwayo Anglo American, Amplats

Wachimba migodi wa Amplats wakigoma mwezi Oktoba

Wachimba migodi wanasema hawakubali pendekezo la kampuni hiyo kuhusu malipo.

Mwezi Oktoba Amplats iliwafukuza makazini wachimba migodi 12,000 kwa sababu walishiriki kwenye mgomo katika migodi ya Rustenberg.

Tangu wakati huo uchimbaji wa dhahabu nyeupe umeathirika sana.

Amplats ni kampuni kubwa ya mwisho ya Afrika Kusini ambayo bado inaathirika na migomo - migomo iliyokuwa na ghasia ambapo watu zaidi ya 50 wamekufa.

Wachimba migodi 34 walipigwa risasi na polisi katika mgodi wa kampuni ya Lonmin mwezi wa Agosti.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.