Mpango kuhusu Mali watayarishwa

Imebadilishwa: 11 Novemba, 2012 - Saa 10:23 GMT

Viongozi wa Afrika Magharibi wanatarajiwa kukutana katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, kukamilisha mipango ya kuwatuma wanajeshi kaskazini mwa Mali.

Mawaziri wa Ivory Coast katika mkutano wa ECOWAS, Nigeria

Mazungumzo hayo yatashughulika na mapendekezo ya kutuma wanajeshi elfu kadha kuwaondoa wapiganaji wa Kiislamu, iwapo juhudi za kufanya majadiliano hazitafanikiwa.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limewasihi viongozi Afrika magharibi kutayarisha mpango huo kufikia mwisho wa mwezi huu.

Mataifa ya Magharibi yamejitolea kutuma vikosi vya kutoa mafunzo kwa majeshi ya Afrika Magharibi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.