Mali ni hatari kwa Afrika

Imebadilishwa: 11 Novemba, 2012 - Saa 14:37 GMT

Rais wa Nigeria ameonya kuwa matokeo yanaweza kuwa mabaya kwa Afrika iwapo wapiganaji wa Kiislamu hawataondoshwa kaskazini mwa Mali.

Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria

Rais Goodluck Jonathan alisema Nigeria inataka kikosi cha jeshi kipelekwe huko haraka.

Alisema wapiganaji wamelifanya eneo kubwa la Mali kuwa halina sheria.

Rais Jonathan alisema hayo kwenye mkutano wa viongozi wa Afrika magharibi wa jumuia ya ECOWAS mjini Abuja, ambako wanajadili mpango wa kutuma wanajeshi elfu kadha Mali iwapo majadiliano na wapiganaji hayatafanikiwa.

Umoja wa Mataifa umetoa idhini kuingilia kati kijeshi nchini Mali.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.