AU kutuma wanajeshi Mali

Imebadilishwa: 14 Novemba, 2012 - Saa 10:26 GMT
Waasi wa Mali

Waasi wa Mali

Muungano wa Afrika AU umeunga mkono mpango wa kuwatuma wanajeshi wa kutunza amani nchini Mali, kusaidia katika harakati za kupamabana na wanamgambo wa Kiislamu walioko Kaskazini mwa nchi hiyo.

Kamati kuu wa muungano huo, imeidhinisha uamuzi uliochukuliwa na Muungano wa Kiuchumi wa nchi za Magharibi mwa Afrika ECOWAS wa kutuma wanajeshi 3,000 kusaidia serikali ya Mali, kupambana na waasi hao.

Mpango huo sasa utawasilishwa kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ili kuidhinishwa kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Wapiganaji wa Kiisalmu na wa kabila la Toureq walichukua uthibit wa eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo baada ya rais wa nchi kuondolewa madarakani kufuatia mapinduzi yaliyofanyika mwezi Machi mwaka huu.

Umoja wa Mataifa umeonya kuwa wapiganaji hao wa Kiislamu wanataka kutekelezwa kwa sheria kali za Kiislamu katika maeneo wanayoyathibiti.

Ripoti ya Umoja huo imesema visa vya ndoa vya lazima, vimeongezeka sawia na wasichana kulazimisha kufanya vitendo vya ukahaba na pia kesi za ubakaji zimeongezeka.

Muungano huo wa ECOWAS unatarajiwa kudumu kwa muda wa miezi sita, awamu ya kwanza ikiwa mpango wa kuwapa mafunzo na kujenga kambi Kusini mwa Mali, kabla ya kuanzisha mikakati ya kijeshi Kaskazini mwa nchi hiyo.

Nchi za Nigeria, Niger na Burkina Faso zimehaidi kutoa wanajeshi hao watakaotumwa nchini Mali.

Baada ya kuidhinisha mpango hupo, kamishna mkuu wa Usalama na Amani wa muungano wa Afrika, Ramtane Lamamra, ametoa wito kwa mataifa mengine ya Kiafrika kutoa wanajeshi zaidi na misaada zaidi ili kufanikisha mpango hu

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.