Mpaka wa Uganda na DRC wafungwa.

Imebadilishwa: 14 Novemba, 2012 - Saa 09:50 GMT
Waasi wa M23

Waasi wa M23

Serikali ya Uganda imetangaza kufunga mpaka wake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika kivuko cha Bunagana.

Hatua hiyo ya serikali ya Uganda inajiri baada ya ripoti moja ya Umoja wa Mataifa kuishutumu Uganda kwa kuwaunga mkono waasi wa M-23 wanaopigana na serikali katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Uganda na Rwanda zimepuuza kabisa ripoti hiyo.

Msemaji wa jeshi la Uganda, Kanali Felix Kulaigye, amethibitisha amri ya kufungwa kwa mpaka huo iliyotolewa na rais wa Uganda, Yoweri Museveni.

Eneo hilo la mpakani la Bunagana ni muhimu kwa usafirishaji bidhaa zinazotumiwa na wapiganaji wa kundi hilo la waasi wa M-23.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.