Suarez haendi kokote

Imebadilishwa: 15 Novemba, 2012 - Saa 18:25 GMT
Luis Suarez

Luis Suarez

Kocha wa livepool Brendan Rodgers amesema nyota wake Luis Suarez atasalia na klabu hiyo na kukariri kuwa hakuna klbau yoyote ambayo imeonyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo.

Klabu ya manchester City imeripotiwa kuonyesha nia ya kumsajili Suarez, 25,. Mapema msimu huu mchezaji huyo kutoka Uruguay alisaini mkataba mpya na klabu hiyo na amekuwa katika hali nzuri ambapo amefunga jumla ya magoli 11 baada ya kucheza mechi kumi na sita.

'' Ikiwa tutampoteza Luis, basi hatutakuwa na washambulizi, na kwa sasa sina uwezo wa kumpoteza yeyote'' alisema Roggers.

Suarez alilipwa kitita cha puani milioni 22.7 wakati alipokihama klabu ya Ajax na kujiunga na klabvu ya Liverpool Januari mwaka wa 2011.

Katika msimu wake wa kwanza na Liverpool, Suarez alifunga magoli 17 baada ya kucheza mechi 39.

Hata hivyo mchezaji huyo amekumba na mizozo kadhaa akiwa England.

Suarez alipatikana na hatia ya kutumia lugha ya ubaguzi wa rangi dhidi ya mlinda lango wa Manchester United Patric Evra, na kupigwa marufuku ya kutoshiriki katika mechi nane.
Vile vile alishutumiwa kwa kutomsalimia Evra wakati wa mechi yao katika uwanja wa Old Trafford.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.