Compaore kukutana na waasi wa Mali

Imebadilishwa: 16 Novemba, 2012 - Saa 10:32 GMT
Viongozi wa Ecowas

Viongozi wa Ecowas

Rais wa Burkina Faso, Blaise Compaore, anatarajiwa kukutana na waakilishi wa waasi wa Kiislamu wanaodhibiti kaskazini mwa Mali, Leo Ijumaa, katika juhudi zake za kutatua mzozo nchini humo.

Mazungumzo hayo yatakayojumuisha Ansar Dine na Tuareg yanajiri huku matayarisho ya kuwatuma wanajeshi Kusini mwa Mali, yakiendelea.

Siku ya Alhamisi, Nigeria ilisema inatarajia kuwatuma wanajeshi wake Kusini mwa Mali, katika muda wa wiki mbili zijazo.

Mkuu wa Jeshi la Nigeria, Ola Ibrahim, ameiambia BBC, kuwa Nigeria, itatoa wanajeshi elfu moja, kati ya zaidi ya elfu tatu waohitajika kutoka Mataifa ya Afrika Magharibi.

Mataifa ya Magharibi pia yamethibitisha yatatoa usaidizi kwa operesheni hiyo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.