EU kutoa mafunzo kwa jeshi la Mali

Imebadilishwa: 16 Novemba, 2012 - Saa 12:46 GMT
Mawaziri wa Muungano wa Ulaya

Mawaziri wa Muungano wa Ulaya

Mawaziri wa mambo ya nchi za kigeni na ulinzi kutoka mataifa matano ya Muungano wa Ulay, EU wameunga mkono pendekezo na wanajeshi wa muungano huo kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Mali ambao wanapambana na wanamgambo wa Kiislamu.

Ujerumani, Italia, Uhispani, Poland na Ufaransa zimetoa taarifa ya pamoja mjini paris zikiunga mkono mpango huo kuhusu Mali.

Mataifa ya Afrika Magharibi yananuia kutuma kikosi cha kijeshi ili kusaidia wanajeshi wa nchi hiyo kumbomba tena eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo kutoka kwa wapiganaji wa Kiislamu walio na uhusiano na kundi la kigaidi la al-Qaeda.

Ikiwa pendekezo hilo litaidhiisha na Umoja wa Mataifa, wanajeshi hao wanatajiwa kuwasili nchini Mali wiki chache zijazo.

Pendekezo hilo linatarajiwa kujadiliwa katika baraza la usalama la Umoja wa Mataofa kabla ya mwisho mwisho wa mwaka huu.

Muungano wa Afrika tayari umeunga mkono mpango wa kutuma wanajeshi 3,300 nchini Mali chini ya muavuli wa muungano wa Kiuchumi wa nchi za Magharibi mwa Afrika Ecowas.

Wapiganaji wa waasi wa Kiislamu na wale wa kabila la Tuareg waliuteka eneo la Kaskazini mwa Mali, baada ya rais wa nchi hiyo kuondolewa mdarakani kupitia mapinduzi ya serikali.

Lakini wapiganaji hao waligawanyika na kutengana na wale wa Tuareg na wamekuwa wakiendeleza mikakati ya kuyathibiti miji zaidi huku wakianzisha utawala wa unaozingatia sheria za Kiislamu maarufu kama Sharia.

Umoja wa Mataifa umeonya kuwa wapiganaji hao wa Kiislamu wamekuwa wakitumia sheria hizo kali za Kiislamu katika maeneo wanayoyathibiti na kuwa visa vya ndoa ya lazima, ukahaba wa lazimana ubakaji vimeongezeka kwa kiasi kikubwa.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.