Israel yalenga ofisi za Hamas Gaza

Imebadilishwa: 17 Novemba, 2012 - Saa 14:05 GMT

Jeshi la wanahewa la Israil limeshambulia kwa mabomu ofisi ya waziri mkuu kutoka chama cha Hamas pamoja na jengo la baraza la mawaziri kwenye ukanda wa Gaza, katika siku ya nne ya mashambulio.

Gaza  ikishambuliwa


Wapalestina 39, wakiwemo watoto kadha, wameuwawa tangu mashambulio hayo kuanza siku ya Jumatano.

Wapiganaji wa Gaza wameendelea kurusha makombora dhidi ya Israil, baada ya kulenga miji ya Tel Aviv na Jerusalem hapo jana.

Hamas imeomba madawa kutoka nchi za Kiarabu.

Israel inasema mashambulio yake yameleta uharibifu mkubwa katika vituo vilioko chini ya ardhi ambako makombora ndiko yanakorushwa.

Waziri wa mashauri ya Nchi za Nje wa Tunisia, ambaye alitembelea eneo la Gaza Jumamosi, alitoa wito kwa viongozi wa Kiarabu - wataokutana baadae mjini Cairo - kumaliza kile alichoita uhasama wa Israel.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.