Mapigani ya waasi yaanza Mali

Imebadilishwa: 17 Novemba, 2012 - Saa 15:49 GMT
Wapiganaji wa waasi nchini Mali

Wapiganaji wa waasi nchini Mali

Wapiganaji wa Kiislamu na wale kabila la Militant Tuareg wamekabiliana vikali Kaskazini mwa Mali.

Waasi haoa wanasema wameanzisha mashambulio dhidi ya vugu vugu na Kiislamu la Movement for Unity and Jihad in West Africa (Mujao) lakini wapiganaji wa kundi hilo wakajibu kwa kufanya mashambulio mazito.

Kwingine waasi wengine na wapiganaji wengine wa Kiislamu wa Ansae Dine, wanafanya mazungumzo katika nchi jirani ya Burkina Faso.

Wanamgambo hao wa Kiislamu wanasema wako tayari kufanya kazi na serikali ya Male ili kumaliza miezi kadhaa ya machafuko kaskazini mwa nchi hiyo.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa linatarajiwa kujadili mpango wa kutuma wanajeshi wa umoja huo wa kutunza amani katika eneo la Kaskazini.

Muungano wa kiuchumi wa nchi za Magharibi mwa Afrika, ECOWAS, umesema kuwa utatuma takriban wanajeshi 3,300 nchini Mali ikiwa Umoja wa Mataifa utaidhinisha pendekezo hilo.

Wapiganji wa Kiislamu na waasi wanaojumuisha wapiganaji kutoka kwa kabila ka Tuareg kwa pamoja wanaojulikana kama National Movement for the Liberation of Azawad (MNLA) wailiuteka eneo la Kaskazini mwa Mali mapema mwaka huu baada ya kukabiliana vikali na wanajeshi wa serikali.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.