Mzozo kati Newcastle na Senegal

Imebadilishwa: 17 Novemba, 2012 - Saa 16:49 GMT
Papiss Cisse

Papiss Cisse

Klabu ya Newcastle, imeelezea masikitiko yake kuhusiana na uamuzi wa shirikisho la mchezo wa soka nchini Senegal, kumzuia Papiss Cisse, kutocheza mechi yao ya leo dhidi ya Swansea.

Mshambulizi huyo, alijiondoa kutoka kwa kikosi cha timu ya taifa ya Senegal, kilichochuana na Niger, mapema wiki hii, kutokana na jeraha la mgongo.

Senegal iliumia sheria ya FIFA kumpiga marufuku mchezaji huyo kutoshiriki katika mechi yoyote kwa muda wa siku tano, kwa misingi kuwa haikupokea ripoti kuhusu hali ya afya ya mchezaji huyo.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotumwa kwa vyombo wa habari na klabu hiyo, haijafurahishwa na uamuzi huo.

Newcastle imesisitiza kuwa iliifahamishwa Senegal kuwa mchezaji huyo hatakuwa katika hali nzuri kuakilisha tafaifa lake wakati wa mechi hiyo ya Jumatano nchini Niger.

Ripoti hiyo imenadi kuwa Cisse alipata jeraha hilo wakati wa mechi yao dhidi ya Westham.

Chini ya sheria ya FIFA iliyotekelezwa na Senegal, mataifa wanachama wake wana uhuru wa kuwapiga marufuku wachezaji wake kutoshiriki katika mechi yoyote kwa muda wa siku tano, ikiwa atakosa kujiunga na timu ya taifa bila sababu nzuri.

Wakati huo huo, Cisse mwenye umri wa miaka 27, amesema kwa sasa anachunguza uwezekano wa kujiondoa kama naodha wa timu hiyo ya taifa ya Senegal.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.