Mswada wa maaskofu wanawake washindwa

Imebadilishwa: 21 Novemba, 2012 - Saa 15:05 GMT

Askofu wa Canterbury anayemaliza muda wake Rowan Williams ameelezea kusikitishwa kwake na kukataliwa kwa mapendekezo ya kuwaruhusu wanawake kuhudumu kama maaskofu.

Amesema uamzi huo hautakuwa wa busara kwa jamii amesema kanisa halikupitisha hatua ya kupinga kujumuishwa kwa wanawake kuwa maaskofu, lakini amesema hakukuwa na suluhu kutoka kwa mungu

Naaye askofu mkuu mpya aliyeteuliwa kuliongoza kanisa la Canterbury, Justin Welby ametaja hatua ya kanisa la Uingereza ya kupinga kutawazwa kwa maaskofu wanawake kama ya kuhuzunisha katika dini hiyo.

Kanisa kuu la Uingereza limekataa kuidhinisha mpango wa kuwatawaza wanawake kama maaskofu, na hivyo kuvunja matumaini yakufanyika kwa mabadiliko ya sheria za kanisa hilo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.