Viongozi wamaliza kuijadili DRC

Imebadilishwa: 24 Novemba, 2012 - Saa 15:51 GMT

Viongozi wa Afrika wamewasihi wapiganaji mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo kuacha mashambulio.

Rais Joseph Kabila alihudhuria mkutano wa Kampala

Mwisho wa mkutano wao mjini Kampala, Uganda, viongozi hao wamewataka wapiganaji wa kundi la M23 waondoke kutoka mji wa Goma waliouteka hivi karibuni.

Viongozi hao piya walimsihi Rais wa Congo, Joseph Kabila, kushughulikia malalamiko ya wapiganaji.

Viongozi wane walihudhuria mkutano huo - Rais Paul Kagame wa Rwanda hajakuwepo.

Walipendekeza kuweka kikosi cha pamoja katika uwanja wa ndege wa Goma kitachokuwa na wanajeshi kutoka Tanzania, jeshi la Congo na M23.

Rwanda inashutumiwa kuwa inawasaidia wapiganaji wa M23 - shutuma inazokanusha.

Baada ya kuuteka mji wa Goma, wapiganaji wamesonga ndani zaidi kwenye ardhi iliyokuwa ikidhibitiwa na serikali.

Mashirika ya misaada yanaonya kuwa hali ya wakaazi inazidi kuwa mbaya.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.