Mabomu yalipuliwa kambini Kaduna

Imebadilishwa: 26 Novemba, 2012 - Saa 07:01 GMT


Jeshi la Nigeria linasema kuwa mabomu yaliyotegwa kwenye magari mawili yamelipuliwa ndani ya kambi karibu na mji wa Kaduna, Kaskazini mwa nchi.

Kanisa la Kaduna liloshambuliwa mwezi Oktoba

Watu kama 11 waliuwawa na 30 kujeruhiwa.

Mshambuliaji wa kwanza alikuwa kwenye basi lilojaa mabomu na aligonga kanisa wakati ibada ya Jumapili ikimalizika.

Dakika 10 baadaye gari lililotegwa bomu lililipuka nje ya kanisa.

Jeshi la Nigeria limelaumu kundi la wapiganaji wa Boko Haram.

Msemaji wa jeshi alisema mashambulio hayo ndani ya kambi ilioko Jaji, yanatia aibu.

Boko Haram inapigana kuipindua serikali ya Nigeria, ili kuweka sheria kali za Kiislamu.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.