Krismasi yaja mapema kwa wanajeshi Afghanistan

Imebadilishwa: 27 Novemba, 2012 - Saa 09:07 GMT

Muigizaji wa James Bond Daniel Creig, alizuru Afghnaistan hivi maajuzi

Hebu tafakari hali ya Afghanistan! Taarifa zote zinazotoka huko huwa ni za kusikitisha na kutia majonzi, kwani leo utasikia, mauaji ya watoto, kesho utasikia polisi walishambuliwa, au hata wanajeshi wa NATO wameshambuliwa. Ndizo simulizi za Afghanistain.

Lakini licha ya hayo yote, kuna mtangazaji mmoja yuko tayari kupeperusha matangazo kutoka huko na hasa kutoka katika kambi ya jeshi.

Mtangzaji wa BBC Greg James,wa (Radio 1) ambayo ni moja wapo ya vituo vya redio vya BBC nchini Uingereza, anajiandaa kupeperusha kipindi chake cha redio kutoka nchini Afghanistan, kwa siku tano kuanzia Jumatatu Disemba tarahe kumi.

James atatangaza kutoka kambi ya jeshi ya Uingereza ambako, ataandamana na wanajeshi na hata kutuma ujumbe wa krismasi kutoka kwa wanajeshi hao.

Kipindi chake kitapeperushwa kuanzia saa kumi hadi saa moja kila siku na kitaendeshwa kwa usaidizi wa wanajeshi wa Uingereza.

Lengo la Greg James ni kuonyesha ambavyo jeshi linaendesha shughli zao kutoka kambini katika nchi inayokumbwa na vita.

" Nina furaha sana kutangaza kutoka Afghanistan na kuonyesha wanajeshi kuwa tunatathmini kazi yao,'' alisema Greg.

" Napenda changamoto kama hizi na itakuwa fursa kwangu kuona ambavyo jeshi hupeperusha matangazo yake kutoka kambini.''

Msanii wa redio 1 Greg James

" Nafahamu sio rahisi, lakini nafahamu kuwa muigizaji wa filamu maarufu ya James Bond, Daniel Craig alizuru kambi hiyo wiki jana najua sio kipindi rahisi kufuata kama sinema ya James bond, au? alisema Greg

Sio mara ya kwanza kwa watangazaji wa redio kupeperusha matangao kutoka nchini Afghanistan.

Mkuu wa vipindi katika Radio 1 alisema ni matumaini yao kwamba Greg ataonyesha mazingira wanamofanyia kazi wanajeshi na pia kupeperusha ujumbe wa wanajeshi kwa familia zao wakati wa krismasi.''

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.