Tisho kwa watoto na wanawake Jonglei

Imebadilishwa: 27 Novemba, 2012 - Saa 07:48 GMT

Wanawake wanakabiliwa na wakati mgumu hasa wakati huu wa kiangazi

Ripoti mpya iliyochapishwa na shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka, Medecins sans Frontieres, imeonya kuwa wanawake na watoto katika jimbo la Jonglei nchini Sudan Kusini, wanazidi kulengwa katika mapigano ya kikabila.

Shirika la MSF linasema watoto wengi wanatekwa nyara na wakati mwingine kuuwawa wakati wa wizi wa mifugo ambao husababisha mapigano ya kikabila.

Ripoti hiyo kadhalika inaelezea uharibifu wa taasisi chache za kutoa huduma za afya katika jimbo hilo.

Kwa mujibu wa MSF, jimbo la Jonglei linakabiliwa na hali ya dharura wakati huu ambapo ni msimu wa kiangazi , ikizingatiwa kuwa jimbo hilo,lina viwango vya juu vya umaskini.

Kuna hofyu kuwa hali hii huenda ikachochea zaidi mapigano na watu wengi kuachwa bila makao.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.