Rasimu ya katiba Misri licha ya zogo

Imebadilishwa: 29 Novemba, 2012 - Saa 09:20 GMT

Purukushani katika medani ya Tahrir wakati wa maandamano dhidi ya rais Mursi

Kiongozi wa baraza linaloandika katiba mpya ya Misri amesema kuwa pindi tu stakabadhi hiyo itakapokamilika ikiwa katika hali rasimu, huenda wananchi wakahitajika kushiriki katika kura ya maamuzi baadaye Alhamisi.

Ikiwa itaidhinishwa na Rais wa Misri Mohamed Mursi, katiba inaelekeza wananchi washiriki katika kura ya maamuzi.

Katika mahojiano na gazeti la Times, Bwana Musri alipa kuwa atayaachilia mbali mamalka mapya aliyojikabidhi katiba mpya itakapoanza kutumika.

Taarifa hii inakuja huku mahakama ya kikatiba ikiashiria kuwa itaamua Jumapili ikiwa itavunja baraza hilo

Idara ya mahakama ya Misri iko katika mvutano na Rais wa nchi hiyo Mohammed Mursi na wafuasi wake wa kiisilamu baada ya bwana Mursi wiki jana kupitisha sheria inayompa mamlaka kupindukia.

Hofu kuhusu rasimu ya katiba

Hatua hiyo ya rais imezua zogo kote nchini humo.

Huku maandamano yanayopinga hatua ya rais yaliendelea kote nchini , maafisa katika baraza hilo walisema kuwa wanakamilisha rasimu ya katiba licha ya bwana Mursi kuliongezea muda ili kukamilisha rasimu hiyo mwezi Februari.

Kulingana na vyombo vya habari vya serikali, kura ilitarajiwa kupigwa siku ya Alhamisi kuhusiana na mada hiyo.

Waandamanaji walipinga hatua ya rais kujilimbikizia mamlaka

Mwandishi wa BBC nchini Misri, Jon Leyne, anasema kuwa kutolewa kwa katiba katika mazingira haya ya zogo, huenda ikawa tisho kubwa kwa usalama.

Kiongozi wa upinzani na aliyekuwa mwenyekiti wa Jumuiya ya kiarabu,Amr Moussa aliambia waandishi wa habari kuwa ni upuzi mtupu, na mojawapo ya hatua ambazo hazipaswi kuchukuliwa kabisa ikizingatiwa hasira ya watu juu ya baraza la kikatiba.

Baraza la kikatiba lina wanachama wengi wa Muslim Brotherhood na wanasiasa wengine wenye msimamo mkali na ambao wanamuunga rais Mursi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.