200 wajeruhiwa wakitafuta kazi Tunisia

Imebadilishwa: 29 Novemba, 2012 - Saa 07:28 GMT

Mmoja wa waliojeruhiwa wakitafuta ajira huko Tunisia

Zaidi ya watu mia mbili walijeruhiwa huko Tunisia Jumatano katika siku ya pili ya maandamano jijini Siliana kilomita mia moja Ishirini kutoka katika jiji kuu la Tunis.

Waandamanaji hao walikuwa wakimtaka gavana wa eneo hilo kujiuzulu, kutaka msaada wa kiuchumi na vile vile kushinikiza watu kumi na wanne waliokamatwa katika ghasia za Aprili kuachiliwa.

Maafisa wa usalama walitumia gesi ya kutoa machozi na risasi za mipira kuwatwanya watu waliokuwa wanataka ajira. Pia kulikuwa na ripoti za watu kutibiwa baada ya kupata majeraha ya risasi.

Vyama vya wafanyakazi vimeitisha maandamano zaidi baadaye leo.

Tunisia ndiyo ilikuwa kitovu cha mapinduzi ya kiraia katika nchi za Kiarabu ambapo wananchi walimng'oa mamlakani rais wao wa muda mrefu Januari mwaka 2011.

Kususia chakula

Waziri mkuu wa nchi hiyo Hamadi Jebali amekataa wito wa waandamanaji kuwa aondoke mamlakani akisema kupitia televisheni kuwa Gavana hang'atuki

Mwandishi wa BBC Sihem Hassaini ambaye yuko mjini Tunis, anasema kuwa maandamano hayo ni ya hivi karibuni katika msururu wa maandamano mengine ya watu wanaeolezea kukerwa na ukosefu wa mageuzi ya kuridhisha tangu mapinduzi ya kiraia kufanyika.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.