Ghasia zaidi zatokea kaskazini Nigeria

Imebadilishwa: 2 Disemba, 2012 - Saa 16:30 GMT

Kumetokea ghasia kadha kaskazini mwa Nigeria.

Ramani ya jimbo la Bauchi, Nigeria

Katika eneo la mbali kaskazini-mashariki mwa nchi, watu wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa kundi la wapiganaji wa Kiislamu, Boko Haram, walishambulia kanisa, kituo cha polisi, na ofisi za uhamiaji na ushuru katika mji wa Gamboru-Ngala, karibu na mpaka wa Cameroon.

Askari polisi wawili waliuwawa.

Piya kumetokea mapambano baina ya watu waliokuwa na silaha na askari wa usalama kwenye mji wa Azare, katika jimbo la Bauchi, kaskazini mashariki mwa nchi.

Wakaazi wa huko wanasema washambuliaji wawili waliuwawa na wa tatu amejificha ndani ya nyumba ambayo sasa imezingirwa na polisi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.