Papa Benedict kwenye Twitter

Imebadilishwa: 3 Disemba, 2012 - Saa 08:45 GMT

Papa anatarajiwa kuanza kutumia mtandao wa kijamii Twitter kuwasiliana na waumini

Papa Benedict anafungua akaunti katika mtandao wa kijamii,Twitter, katika jitihada ya kusambaza ujumbe wa kanisa katoliki.

Taarifa kuhusu akaunti hiyo itatolewa baadaye hii leo katika mkutano na waandishi habari, lakini duru kutoka Vatican zinasema huenda asiandike mwenyewe ujumbe kwenye akaunti hiyo.

Wanasema Papa Benedict anapendelea kuandika kwa mkono kuliko kutumia tarakilishi.

Kanisa hilo la katoliki tayari linatumia mitandao kadhaa ya kijamii na hivi karibuni limezindua mtandao mkuu unaounganisha mitandao ya kanisa hilo kote ulimwenguni.

Wakatoliki kote duniani, wataweza kuwasilina na Papa kupitia Twitter wakati akaunti hiyo itakapozinduliwa rasmi.

Papa Benedict anataka kuitumia akaunti hiyo kuwasiliana na wakatoliki kote duniani.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.