Milolongo mirefu kwenye uchaguzi wa Ghana

Imebadilishwa: 7 Disemba, 2012 - Saa 14:09 GMT

Wadadisi wanasema ushindani utakuwa mkali kati ya wagombea

Milolongo mirefu imeshuhudiwa katika vituo vya kupigia kura kote nchini Ghana huku watu wakimchagua rais mpya pamoja na wabunge wapya.

Katika baadhi ya maeneo, upigaji kura ulicheleweshwa kwa masaa kadhaa, ingawa ulionekana kuendelea vyema kwa amani, bila matatizo.

Wachunguzi wanatabiri kuwa ushindani utakuwa mkubwa kati ya rais wa sasa John Dramani Mahama na Nana Akufo-Addo, ambaye babake aliliongoza taifa hilo katika miaka ya sabini.

Rais Mahama anawania muhula wake wa kwanza ofisini baada ya kuchukua hatamu za uongozi mwezi Julai kufuatia kifo cha ghafla cha mtangulizi wake John Atta Mills.

Duru zinasema kuwa ushindani utakuwa mkali sana hasa baada ya bwana Akufo-Addo kufanya vyema katika uchaguzi uliopita.

Wapiga kura wametumia mitandao ya kijamii kutoa uhamasisho kuhusu uchaguzi wa amani na huku wengi wakielezea kuwa na hamasa kubwa

Ghana kwa miaka mingi imekuwa kipenzi cha waekezaji katika eneo ambalo lenye historai ya migogoro ya kisiasa na hata mapinduzi.

Moja ya mada inayojadiliwa miongoni mwa wapiga kura imekuwa mapato yanayotakana na mafuta na ambavyo nchi inaweza kuyatumia vyema.

Rais wa sasa bwana Mahama, ameahidi kuboresha viwango vya maisha katika nchi hiyo ambayo raia wa kipato cha chini hupata chini ya dola nne kwa siku.

Mpinzani wake bwana Akufo-Addo, anayeunga mkono soko huru, ameahidi kutumia mapato yanayotokana na mafuta kuendeleza sekta ya elimu.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.