Jeshi la Misri laonya wanasiasa

Jeshi la mIsri laweka kizuizi mbele ya ikulu ya rais

Jeshi la Misri limeonya matokeo mabaya iwapo pande zinazolumbana kisiasa zitashindwa kutatua hitilafu zao kwa mazungumzo.

Katika taarifa iliyotolewa kwenye televisheni ya taifa msemaji alieleza kuwa jeshi halitavumilia ghasia zaidi; ingawa duru za jeshi zilisisitiza baadae kwamba hiyo haimaanishi kuwa jeshi litaingilia kati na kuchukua madaraka.

Maandamano yameendelea nje ya ikulu ya rais yakimtaka Rais Mohammed Morsi abatilishe uamuzi wake wa kujizidishia madaraka na kutaka kura ya maoni ifanywe kuhusu katiba mpya.

Upigaji kura ya maoni kwa Wamisri walioko nchi za n'gambo sasa umeahirishwa.

Hapo jana maelfu ya wapinzani mjini Cairo walitaka tena kuwa shughuli yote ifutwe.