Mugabe ataka kampuni ziwe za wazalendo

Imebadilishwa: 8 Disemba, 2012 - Saa 10:28 GMT

Rais Robert Mugage wa Zimbabwe ametoa wito kuwa makampuni yote ya kigeni yalioko nchini yamilikiwe kikamilifu na wananchi.

Rais Robert Mugabe

Amesema hayo wakati Zimbabwe inajitayarisha kwa matukio mawili muhimu - kura ya maoni kuhusu katiba mpya itayofuatiwa na uchaguzi mkuu.

Rais Robert Mugabe atatimia miaka 89 mwezi wa Februari lakini umri haukumlainisha.

Ijumaa mpigania ukombozi huyo wa zamani alihutubia mhadhara wa wafuasi 5,000 wa chama chake cha Zanu-PF katika mji wa Gweru.

Ujumbe wake ulikuwa mkali kama kawaida.

Ametoa wito kuwa sheria ya sasa inayoruhusu Wazimbabwe kumiliki angalau asili-mia-51 ya makampuni ya kigeni ibadilishwe kabisa.

Alisema ameiambia wizara ya migodi ibadilishe sheria ya sasa inayoruhusu wageni kubaki na asili-mia-49 ya makampuni.

Alisema "Nimeiambia wizara tuwape nafasi watu wetu.

Tuwe na wachimbaji wetu, wana-teknolojia mpya, na wanasayansi.

Wacha wao wachimbe.

Wacha tumiliki haya makampuni kikamilifu"

Matamshi ya Bwana Mugabe yanaweza kuwa ishara kuwa anataka kurejea tabia yake ya kufanya kampeni kwa kuonesha uzalendo kabla ya uchaguzi wa mwakani.

Uchaguzi hautafanywa hadi katiba mpya imekubaliwa.

Lakini Rais Mugabe anasema atasonga mbele vovote vile, hata kama hatafikia makubaliano na chama cha upinzani cha MDC cha Morgan Tsvangirai.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.