Asakwa kwa kuwaharibu watoto Uganda

Imebadilishwa: 11 Disemba, 2012 - Saa 08:27 GMT

Uganda inawataka polisi wa Interpol kumkamata mshukiwa

Polisi nchini Uganda wamelitaka shirika la polisi wa kimataifa la Interpol, kutoa kibali cha kukamatwa kwa meneja wa timi moja ya soka nchini humo kwa madai ya kuwalawiti wavulana wadogo pamoja na kuwaharibu watoto wa kike.

Madai dhidi ya Chris Mubiru yameripotiwa kwa kina katika gazeti la udaku la Red Pepper tangu siku ya Ijumaa pamoja na kile linachosema ni picha za vitendo vya meneja huyo.

Ingawa madai haya yanahusika zaidi na vitendo vya kuwaharibu watoto, kisa hiki kimetokea wakati bunge la Uganda linajiandaa kwa mjadala kuhusu mswaada tatanishi wa kupinga vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.

Picha hizo za kushtua, zinaonyesha mwanamume akiwa anawalawiti watoto zikiwa kwenye ukurasa wa kwanza wa gazeti hilo kwa siku ya nne mfululizo.

Picha za hizo zinasemekana kutoka kwa mshukia mwenyewe alizopiga akifanya vitendo vyake, ingawa bado kuna tashwishi kuhusu uhalali wa picha hizo.

Mubiru, ambaye ni meneja wa timu moja ya soka mjini Kampala, bado hajajibu tuhuma hizo.

Polisi sasa wanasema wanashuku alitoroka nchini humo Jumamosi asubuhi na anaaminika kuwa nchini marekani au Canada.

Wanataka waranti ya kimataifa kumkamata.

Umma wa Uganda pia umetoa kauli kali kuhusu tuhuma hizi. Watu wengi katika vyombo vya habari na pia kwenye mitandao ya kijamii, wametaka hatua kuchukuliwa dhidi ya mshukiwa.

Inaarifiwa taarifa hiyo imeweza kupiga jeki mjadala kuhusu mswaada unaoharamisha mapenzi ya jinsia moja ambao unatarajiwa kutoa adhabu ya kifungo kwa wale watakaopatikana na hatia.

Huenda ukapitishwa wiki hii ingawa serikali inasisitiza kuwa mshukuwa hafungwi kwa misingi ya jinsia yake wala sio kwa sababu ya mswaada huu unaojadiliwa.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.