Utahitaji viza kusafiri Rwanda.Kwa nini?

Imebadilishwa: 11 Disemba, 2012 - Saa 10:47 GMT

Rais wa Rwanda Paul Kagame. Rwanda ina sifa nzuri ya kukaribisha waekezaji wa kigeni

Watawala nchini Rwanda wametangaza uamuzi wao kutoa viza kwa waafrika wanaokwenda nchini humo au hata kupitia huko wakielekea katika nchi zinginezo.

Mabadiliko hayo yanatarajiwa kuanza kutekelezwa mwezi ujao. Sasa nini kimechochea mageuzi haya na kwa nini wakati huu?

Serikali ya Kigali inasema kuwa hatua hii inalenga kuwafanya watalii zaidi kuingia nchini humo. Kulingana na idara ya uhamiaji nchini humo, uamuzi huu utasaidia pia kuondoa tatizo la muda mrefu linaotumiwa na watu wanaoomba viza kutoka katika mataifa mengi ya Afrika.

Kwa wakati huu,kila mwafrika isipokuwa wale wanaotoka katika nchi ambazo hazihitaji viza kuingia Rwanda, watahitajika kujaza fomu hiyo ya kuomba viza kabla ya kuingia Rwanda.

Itawagharimu wasafiri dola thelathini kwa siku thelathini nchini humo. Ingawa watu wataanza kulipia viza hiyo,kuanzia Januari mwaka 2013, waafrika wanaosafiri kuelekea Rwanda, wanatahitajika kupata fumo za viza katika viwanja vya ndege au katika sehemu yoyote ya mpaka na nchi hiyo.

Msemaji wa idara ya uhamiaji ya Rwanda anasema kuwa hatua hii pia inalenga kuendeleza umoja wa kiafrika kati ya nchi husika.

Rwanda tayari, ina sifa nzuri kimataifa kwa kuwa nchi nzuri kwa waekezaji. Ingawa nyingi ya pesa inazopata Rwanda zinatoka kwa nchi za kigeni. Lakini kufuatia uamuzi huo mpya, watawala wanasema wanalenga kuwavutia wageni kutoka kote barani.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.