Nigeria yazindua mchezo wa 'Monopoly'

Imebadilishwa: 12 Disemba, 2012 - Saa 12:46 GMT

Mchezo wa Monopoly

Makala ya kwanza Afrika ya mchezo mashuhuri sana wa Monopoly, ilizinduliwa mapema wiki hii mjini Lagos Nigeria.

Kibao ambacho mchezo huo unachezewa , kilisalia kuwa siri kubwa sana hadi kilipozinduliwa, kikiwa ni mchoro wa kisiwa kiitwacho 'Banana Island' kilichosukwa kwa mikono, ili kuwakilisha mtaa wa kifahari wa Nigeria.

Picha halisi ya kibao hicho kwenye mchezo wowote wa Monopoly, huwa ni ya mtaa wa kifahari wa London ujulikanao kama Mayfair.

Picha ya mtaa ya mabanda iliyoko juu kwenye ngazi zilizo kwa wangwa juu ya mji katika kibao hicho ilikuwa ya bei nafuu sana kupatikana wakati wa kutengezwa kwa kibao chenyewe.

Ikiwa mchezo wa Monopoly ungetengezwa kwa nchi zingine za Afrika, unadhani ni picha gani ingechukua mahala pa mtaa wa Mayfair?

Kwa Nairobi je unadhani Mayfair ingweza kuwa Muthaiga au Village Market? Je ingekuwa mitaa ya mabanda ya Kibera au Mathare ambayo inawerza kununuliwa kwa bai nafuu zaidi? Nini maoni yako kwa magwiji wa mchezo wa Monopoly? Tupe maoni yako kwenye ukrasa wetu wa facebook...bbcswahili

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.