Kgalema Motlanthe kumenyana na J.Zuma

Imebadilishwa: 13 Disemba, 2012 - Saa 13:10 GMT

Kgalema Motlanthe (Kushoto) na rais Jacob Zuma

Msemaji wa makamu wa rais wa Afrika kusini Kgalema Motlanthe amesema amekubali uteuzi wake kugombea uongozi wa chama tawala nchini humo cha African National Congress.

Msemaji huyo Thabo Masebe amesema bwana Montlanthe atagombea kiti cha urais cha ANC, makamu wa rais na nyadhifa nyingine .

Atawania kiti hicho wiki ijayo ambapo atakabiliana na rais wa sasa wa Afrika kusini Jacob Zuma katika mkutano wa chama utakaofanyika Bloemfontein.

Waandishi wa habari wanasema yeyote atakayekuwa kiongozi wa ANC atakuwa na nafasi nzuri ya kuwa rais ajae katika baada ya uchaguzi wa mwaka 2014

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.