Mahakama ya Misri yamfunga mwana blogu

Imebadilishwa: 13 Disemba, 2012 - Saa 07:44 GMT
Mahakama ya Katiba Misri

Mahakama ya Katiba Misri

Mahakama moja nchini Misri imempa mwana blogu mmoja kifungo cha miaka mitatau gerezani kwa kukufuru na kudharau dini.

Alber Saber alikamtawa mwezi wa Septemba baada ya majirani kumnyooshea kidole cha lawama kwama ndiye aliweka kilinganishi cha mtandao kilichoashiria sinema iliyoidhihaki dini ya Kiisilamu, na iliyosababisha maadamano makali katika ulimwengu wa Kiisilamu.

Bwana Saber, ambaye haamini mungu yeyote na anayetoka familia ya Kikristo ya dhehebu la Coptic, anaweza kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo iwapo atalipa dola 167 kama dhamana.

Kesi hii inazua maswala nyeti kuhusu uhuru wa maoni wakati ambapo raia wa Misri wanajiandaa kupiga kura ya maoni kuhusu katiba rasimu.

Wito aachiliwe

Wateteaji haki za kibanadamu wametoa wito Bwana Saber aachiliwe.

Kumekuwa na kesi kadhaa zinazohusu kukufuru nchini Misri katika miaka miwili tangu Hosni Mubarak apinduliwe. Wengi wa washtakiwa ni wa dhehebu la Copts, ambao ni asilimia 10 ya idadi ya watu nchini.

Ingawaje kumkufuru Mungu limekuwa kosa la jinai kwa miaka mingi, Kifungu 44 cha katiba rasimu kina kifungu maalum kinachopiga marufu kashfa dhidi ya manabii.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.