''Syria yabanwa na waasi'' yasema Urusi

Imebadilishwa: 13 Disemba, 2012 - Saa 11:20 GMT

Wanamgambo wa Free Syrian Army wakimkashifu Rais Al-Assad

Kuna uwezekano kwamba serikali ya Syria inaweza kushindwa na majeshi ya upinzani wakati wowote ule, naibu waziri wa masuala ya kigeni wa Urusi amesema.

Wanajeshi wa rais Bashar al-Assad "wanazidi kupoteza maeneo zaidi kila wa leo", Mikhail Bogdanov alisema Alhamisi, kulingana na mashirika ya habari ya Urusi.

Urusi imekuwa mmojawapo wa washirika wakuu wa serikali ya Bwana Assad.

Wakati huohuo, Urusi inafanya mipango ya kujitayarisha kuwahamisha maelfu ya Warusi toka Syria, Bwana Bogdanov alisema.

Mlipuko

"Kwa kweli hatuwezi kutupilia mbali uwezekano wa kwamba waasi wa Syria wanaweza kushinda," Bwana Bogdanov alisema.

Nchini Syria kwenyewe, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti kutokea kwa mlipuko katika eneo la Qatana, jijini Damascus, ambalo limewaua watu 16, wakiwemo watoto saba.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.