Athari za msaada wa kijeshi kwa Mali

Imebadilishwa: 14 Disemba, 2012 - Saa 10:01 GMT

Waasi wa Tuareg nchini Mali

Nyaraka kuhusu mipango ya siri ya Umoja wa Mataifa zilizofichuliwa kwa BBC zimeelezea athari ya jeshi la kigeni kuingilia mzozo wa kisiasa nchi humo.

Nyaraka hizo zinasema kuwa ikiwa jeshi litaingia nchi humo kupambana na makundi ya waasi, huenda likaongeza idadi ya watu walioachwa bila makao kufuatia mgogoro wa kisiasa unaokumba taifa hilo.

Mipango iliyopendekezwa na mashirika ya misaada ya Umoja huo, inasema kuwa kuingilia mzozo huo huenda kukapandisha idadi ya wale walioachwa bila makao hadi watu laki nane.

Mwandishi wa BBC anasema kuwa athari hizo za msaada wa kijeshi kwa Mali huenda zikachochea juhudi zaidi kutoka kwa wale wanaotaka makubaliano kuafikiwa kati ya makundi hayo na serikali.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.