Kiongozi wa upinzani Sudan akamatwa

Imebadilishwa: 14 Disemba, 2012 - Saa 09:04 GMT

Ramani ya Sudan

Mwenyekiti wa Muungano wa vyama vya upinzani nchini Sudan amekamatwa na maafisa wa serikali.

Farouk Abu Issa alisema kuwa alizuiliwa baada ya kurejea nyumbani kutoka katika mkutano wa hadhara .

Bwana Issa ni kiongozi wa muungano wa vyama vya upinzani nchini Sudan na haijulikani kwa nini alikamatwa.

Duru zinasema alikuwa anaondoka kwenye mkutano na kupinga mauaji ya wanafunzi wanne katika eneo la Darfur

Inaarifiwa alilaumu serikali kwa mauaji hayo yaliyofanyika tarehe saba mwezi huu katika chuo kikuu cha na kuitaka kuyachunguza Al-Gazira na kuitaka kuyachunguza mara moja.

Wanaharakati wanasema kuwa wanafunzi hao waliuawa baada ya kushiriki maandamano ya kupinga hatua ya uongozi wa chuo kikuu kukataa kuwaondolea malipo ya karo wanafunzi kutoka Darfur kulingana na makubaliano yaliyoafikiwa kwenye mkataba wa amani wa Doha kuhusu Darfur.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.