Mandela kafanyiwa uperesheni wa kibofu

Imebadilishwa: 15 Disemba, 2012 - Saa 16:39 GMT

Ikulu ya rais wa Afrika Kusini inasema kuwa Nelson Mandela amefanyiwa uperesheni mjini Pretoria, kutolewa mawe ndani ya kibofu nyongo na anasemekana anaendelea vizuri.

Nelson Mandela

Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini mwenye umri wa miaka 94, alilazwa hospitali juma moja lilopita kutibiwa mapafu, na ukaguzi ukaonesha mawe hayo kwenye kibofu.

Katika taarifa iliyotolewa na serikali, imearifiwa kuwa madaktari waliamua kushughulika na mapafu yake Bwana Mandela kwanza, kabla ya kufanyiwa upersheni wa Jumamosi.

Wakuu wa Afrika Kusini wamelaumiwa kuwa hawakuwa wakieleza hali ya Bwana Mandela, ambayo imechochea wasi-wasi zaidi kuhusu afya yake.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.