Upinzani umeitisha maandamano zaidi

Imebadilishwa: 17 Disemba, 2012 - Saa 17:09 GMT
Shughuli ya kuhesabu kura

Shughuli ya kuhesabu kura Misri

Upinzani mchini Misri, umetoa wito kwa raia wa nchi hiyo kuandamana baada ya Waislamu kudai kuwa wapiga kura wengi wameidhinisha katika kilelezo katika duru ya kwanza ya kura ya maoni.

Chama cha National Salvation Front kimetoa wito kwa raia kuandamana siku ya Jumanne, kuteta uhuru na haki zao na kuzuia udanganyigu na wakati huo huo kukataa katiba hiyo kielelezo.

Muungano huo wa upinzani umesema kuwa kuwa na dosari chungu nzima wakati raia walikuwa wakipiga kura siku ya Jumamosi.

Awali, rais Mohammed Morsi wa chama cha Muslim Brotherhood alisema kuwa asilimia 57 ya raia wa nchi hiyo walipiga kura kuunga mkono.

Hata hivyo rais Morsi alisema takwimu hizo sio rasmi.

Raia wa Misri

Raia wa Misri wakipiga kura

Matokeo ya kura hiyo haitajulikana hadi kufanika kwa duru ya pili siku ya Jumamosi.

Upinzani ulikuwa umeshinikiza kura hiyo kuhairishwa kwa sababu, bunge la nchi hiyo lilikuwa limeidhinisha licha ya wabunge wasioegemea upande wowote pamoja na wakristu na wale wasiokuwa na imani katika dini yoyote kuisusia.

Wabunge hao walilalamika kuwa katiba hiyo kielelezo haitalinda vyema haki za kina mama, dini na pia uhuru wa kujieleza.

Nafasi ya mwisho

siku ya Jumapili jioni, chama cha National Salvation Front, kilitoa wito kwa waandalizi wa kura hiyo kuchunguza uwezekano wa shughuli nzima kurudiwa, likisisitiza kuwa kulikuwepo na makosa mengi kama ilivyoripotiwa na mashirika ya kijamii.

Wanasema miongoni mwa dosari hizo ni pamoja na vituo vya kupigia kura kuendesha shughuli hiyo bila idhini na mwongozo kutoka kwa majaji wa mahakama, uamuzi wa maafisa wa mashirika ya kijamii kuchukua nafasi za majaji, na kuwa baadhi ya makaratasi ya kupigia kura hayakuwa yamepigwa muhuri na wawakilishi wa serikali kufanya kampeini ndani ya vituo vya kupigia kura.

Muungano huo pia umedai kuwa Wakristo walinyimwa nafasi ya kushiriki baada ya wengi wao kudai kuzuiliwa na maafisa waliokuwa wakisimamia shughuli hiyo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.