Shirika WHO laonya kuhusu Malaria

Imebadilishwa: 17 Disemba, 2012 - Saa 14:36 GMT
Mtoto anayeugua Malaria Afrika

Mtoto anayeugua Malaria Afrika

Shirika la Afya duniani WHO, limeonya kwamba juhudi za kupambana na ugonjwa hatari wa Malaria zimeonekana kulegea na kwamba mafanikio yaliyopo huenda yakahujumiwa.

Shirika hilo limesema kuna uhaba mkubwa wa pesa za kufadhili juhudi za kutoa kinga, uchunguzi wa mahabara na matibabu ya ugonjwa huo.

Kwa mfano idadi ya neti za kuzuia mbu zinazosambazwa barani Afrika, imepungua na kufikia nusu ya idadi ya neti zilizokuwa zikitolewa miaka miwili iliyopita na hivyo kuwaacha mamilioni ya watu wakiwa katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa huo hatari.

Shirika la WHO linasema linahitaji dola bilioni tatu zaidi ili kuimarisha kampeni yake dhidi ya malaria na pia linatafuta mbinu mpya za kukusanya pesa za kufadhili na kudumisha kampeni hiyo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.