Waziri adai watekaji nyara wamtaka ajiuzulu

Imebadilishwa: 18 Disemba, 2012 - Saa 10:16 GMT
Waziri wa Fedha wa Nigeria

Ngozi Ikonjo Iweala Waziri wa fedha wa Nigeria

Waziri wa fedha wa Nigeria amewalaumu watu waliokasirishwa na matukio ya hivi karibuni kuhusu sakata ya ruzuku ya mafuta kwa kuhusika katika kumtekanyara mamake mzazi.

Mamake Ngozi Ikonjo Iweala, alitekwanyara mapema mwezi huu na kuachiliwa kwake kulitangazwa ijumaa iliyopita.

Waziri huyo wa fedha, aliashiria kuwa waliomteka nyara mamake kwa siku kadhaa walifanya hivyo kwa sababu za kiasiasa.

Bi Iweala amesema watekaji Nyara hao walitaka ajiuzulu baada ya serikali kuchua hatua ya kuzuia malipo kwa mafuta yaliyopunguzwa bei ghali.

Ufisadi katika secta ya mafuta

Sekta ya mafuita nchini Nigeria, ni fisadi zaidi na hivi majuzi waziri wa fedha alisimamisha malipo ya mafuta hayo baada ya kutokea kwa ripoti kuwa nchi hiyo ilikuwa ikipoteza mabilioni ya dola katika kashfa hiyo.

Ni hatua iliyowaudhi wafanyibiashara ambao wanadaiwa walihusika kwa utekeji wa Bi. Okonjo Iweala, mwenye umri wa miaka 83 na itawashangaza raia wengi wa Nigeria wengi kuwa kuwa utekajinyara nchini Nigeria hauhusishwi na siasa.

Visa vya utekaji nyara ni vingi sana katika maeneo ya Kusini mwa Nigeria lakini vingi vimekuwa viitekelezwa kwa nia ya kupata fedha.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.