Wafanyakazi wa afya wawili zaidi wauawa

Imebadilishwa: 19 Disemba, 2012 - Saa 10:25 GMT
Raia wa Pakistan

Raia wa Pakistanwakiomboleza kifo cha wafanyakazi wa afya

Polisi nchini Pakistan wamesema kuwa watu waliojihami kwa bunduki wamewauwa watu wawili wanaohusika katika kampeni ya utoaji chanjo dhidi ya ugonjwa wa kupooza au polio, siku moja tu baada ya wafanyikazi watano wa afya kuuwawa kwa kupigwa risasi.

Msemaji wa shirika la umoja wa mataifa kuhusu watoto UNICEF, amesema kuwa sasa wamelazimika kuahirisha kampeni hiyo kote nchini Pakistan, kutokana na sababu za kiusalama.

Mashambulizi ya hivi punde katika mji wa Peshawar, yamepelekea mauaji ya mwanamke aliyekuwa akisimamia zoezi hilo la utoaji chanjo, dereva wake na mtu aliyekuwa akitoa chanjo.

Viongozi wa Taliban wanasema kampeni hiyo dhidi ya ugonjwa wa polio ni kisingizio cha kufanya ujasuisi dhidi yao.

Serikali ya Pakistan imesema haitakata tamaa katika juhudi za kutokomeza ugonjwa huo nchini humo na imeapa kukabiliana na wapiganaji hao wa Taleban kwa ushirikiano na jamii ya Kimataifa

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.