Kiongozi wa mashtaka hatajiuzulu Misri

Imebadilishwa: 20 Disemba, 2012 - Saa 18:57 GMT
Rais wa Misri

Rais wa Misri Mohammed Morsi

Kiongozi mkuu wa mashtaka ya umma nchini Misri, Talaat Ibrahim, amebadili uamuzi wake wa kujiuzulu, kufuatia maandamano kupinga uteuzi wake.

Vyombo vya habari nchini Misri vinasema, Bwana Ibrahim, amesema, alitoa tangazo hilo kufuatia shinikizo siku ya Jumatatu na sasa anadai ni jukumu la waziri wa haki kuamua ikiwa ataendelea kuhudumu au la.

Ibrahim aliteuliwa na rais Mohammed Morsi mwezi uliopita baada ya mtangulizi wake kufutwa kazi.

Uamuzi wa rais wa kumfuta kazi kiongozi huyo wa mashtaka ya umma, uliwakasirisha majaji ambao walidai kuwa hatua hiyo inahujumu uhuru wa idara ya mahakama.

Uhasama kati ya rais Morsi na wafuasi wa chama cha Muslim Brotherhood umekuwa ukitokota kwa upande mmoja na wanasiasa wasioegemea upande wowote na idara ya mahakama katika upande mwingine.

Mgomo wa Majaji

Raia wa Misri wakipiga kura

Raia wa Misri wakipiga kura

Rais Morsi alijipa mamlaka makubwa kupitia kwa sheria aliysaini tarehe 22 mwezi uliopita, ambao uliipokonya idara ya mahakama uwezo wa kupinga maamuzi yake.

Miongoni mwa maamuzi aliyoyachukua ni kumfuta kazi mwendesha mashtaka mkuu wa umma Abdel Maguid Mahmoud ambaye aliteuliwa na rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak.

Uamuzi huo uliwagadhabisha raia wa nchi hiyo ambao walifanya maandamano kupinga uamuzi huo na kusababisha ghasi kati ya wafuasi wa rais Morsi na wapinzani.

Lakini baada ya maandamano hayo, rais Morsi alifuta sheria hiyo iliyompa mamlaka makubwa lakini hamkumfuta kakzi kiongozi huyo wa mashtaka.

Baada ya uteuzi wake Bwana Ibrahim, alipewa kazi ya kuthamini upya uchunguzi wa mauaji ya waandamanaji wakati rais Bwana Mubarak alikuwa madarakani.

Ibrahim alitangaza kuwa atajiuzulu siku moja nbaada ya awamu ya mwisho ya kura ya maoni kuhusu katiba mpya

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.