Wahamiaji 50 waangamia baharini Somalia

Imebadilishwa: 20 Disemba, 2012 - Saa 18:25 GMT
Habari za hivi punde

Habari za hivi punde

Takriban watu 55 wanaaminika kuzama majini baada ya meli walimokuwa wakisafiria kuzama katika pwani ya Somalia.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wakimbizi UNHCR, limethibitisha tukio hilo.

Shirika hilo la UNHCR, limesema meli hiyo ilikuwa imebeba kupita kiasi wakati ilipopigwa na dhoruba muda mfupi baada ya kuondoka kutoka bandari ya Bossasso, Kaskazini Mashariki mwa Somalia.

Meli hiyo inaaminika kuwa ilikuwa inaelekea Yemen na ilikuwa imebeba wahamiaji haramu kutoka Ethiopia na Yemen.

Umoja wa Mataifa umesema kuwa ajali hiyo ndiyo mbaya zaidi katika Guba ya Aden tangu Februari mwaka wa 2011 wakati wahamiaji haramu 57 kutoka Somalia walipozama baharini.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.