UM umeidhinisha kutumwa wanajeshi Mali

Imebadilishwa: 21 Disemba, 2012 - Saa 10:31 GMT
Wapiganaji wa Tuareg

Wapiganaji wa Tuareg nchini Mali

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha kutumwa kwa wanajeshi wa Muungano wa Afrika nchini Mali, kujaribu kuwatimua wapiganaji wa Kiislamu, Kaskazini mwa nchi hiyo.

Baraza hilo lilipitisja azimio hilo kwa kauli moja na kuipa mamlaka jeshi hilo kuhudumu katika eneo hilo kwa muda wa mwaka mmoja.

Azimio hilo pia limeweka masharti kadhaa kwa serikali ya Mali, ikiwa ni pamoja na kutekeleza mabadiliko ka kisiasa na kuimarisha mafunzo kwa wanajeshi wake.

Makundi yaliyojihami, baadhi yao yakiwa na uhusiano na kundi la kigaidi la Al-Qaeda, lilitwaa uthibitiwa eneo hilo la Kaskazini mwa Mali, baada ya mapinduzi mwezi Machi kuwa kuanza utekelezwaji wa sheria kali za Kiislamu maarufu kama Sharia.

Wapiganaji wa Tuareg

Wapiganaji wa Tuareg nchini Mali

Muungano wa Kiuchumi wa nchini za Afrika Magharibi Ecowas, umesema wanajeshi wapatao 3,300 wako tayari kwenda nchini Mali, lakini operesheni hiyo haitarajiwa kuanza kabla ya Septembwa mwaka wa 2013.

Azimio hilo lililochapishwa na Ufaransa, limeweka mpango wa hatua wa kuiunganisha taifa hilo la Mali.

Muungano wa Ulaya EU na wanachama wengine wa Umoja wa Mataifa, wamepewa jukumu la kusaidia katika harakati za kujeshi upya jeshi la Mali, ambalo lilisambaratika baada ya watu wa kabila la Tuareg na wapiganaji hao wa waasi kuuteka eneo la Kaskazini.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.