Al-Qaeda ilihusika na utekaji nyara

Imebadilishwa: 21 Disemba, 2012 - Saa 11:21 GMT
Rais wa Ufaransa

Rais wa Ufaransa Francois Hollande

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, amesema kuwa wapiganaji wa Al-Qaeda, au kundi ambalo lina uhusiano nalo ndilo lililohusika na utekaji nyara wa mhandisi mmoja raia wa Ufaransa nchini Nigeria.

Idara ya polisi nchini Nigeria imesema kuwa, kundi moja la watu 30 waloikuwa wamejihami kwa silaha walimteka nyara mhandisi huyo kutoka nyumbani kwake Kaskazini mwa nchi hiyo.

Shambulio hilo lilitokea katika jimbo la Katsin, ambalo liko katika mpaka wa nchi hiyo na Niger, ambako wapiganaji wa Al-Qaeda walioko Kaskazini mwa Afrika wanajulikana kuhudumu.

Wapiganaji wa Kiislamu nchini Nigeria hawajafanya mashambulio mengi katika jimbo hilo la Katsina.

Makundi ya kutetea haki za kibinadam yanasema, kundi la Boko Haram, ambalo linapigana kushinikiza kutumika kwa sheria za Kiislamu nchini Nigeria, limefanya mashambulio ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 3,000, tangu mwaka wa 2010, katika eneo hilo la Kaskazini mwa Nigeria.

Mwandishi wa BBC nchini Nigeria hata hivyo anasema kundi hilo mara nyingi huwa haliwateki nyara watu.

Makundi ya Kiislamu ambayo yanahusishwa na kundi la kigaidi la Al-Qaeda limetwaa uthbiti wa eneo la Kaskazini mwa Mali tangu mwezi Aprili mwaka huu.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.