Baragoi Kenya wavamiwa na kuporwa mifugo

Imebadilishwa: 22 Disemba, 2012 - Saa 17:03 GMT

Habari kutoka Kenya zinasema watu wanaotuhumiwa kuwa majambazi wamevamia kijiji kimoja karibu na mji wa Baragoi, kaskazini magharibi mwa Kenya na kuiba mamia ya mifugo.

Ramani ya Kenya

Majambazi hao karibu mia mbili wanasemekena kuwa na silaha nzito.

Watu wengi wameripotiwa kuhama eneo hilo.

Zaidi ya polisi arobaini waliuawa na wezi wa mifugo katika eneo hilo la Baragoi mwezi Novemba mwaka huu.

Bunge la Kenya, Ijumaa liliitaka serikali kuunda Tume ya uchunguzi kuhusu kuuawa kwa polisi, tukio baya kabisa kuwahi kutokea katika historia ya nchi hiyo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.