Wapiganaji wa CAR wasonga mbele

Imebadilishwa: 23 Disemba, 2012 - Saa 17:05 GMT


Wapiganaji katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wameuteka mji wa Bambari, mji wa tatu kwa ukubwa.

Rais Francois Bozize

Huo ni mji wa sita kutekwa na wapiganaji hao tangu kuanza kupigana awali mwezi huu, na ndio karibu kabisa na mji mkuu, Bangui, kwa wapiganaji hao kuwahi kufika.

Msemaji wa shirika la msaada wa matibabu, Medecins Sans Frontieres, ameeleza kuwa watu wengi wamekimbia makwao kwa sababu ya mapigano, pamoja na yale maeneo ambayo bado yanadhibitiwa na jeshi la serikali.

Wapiganaji hao - wanaoitwa ushirikiano wa Seleca - wanataka kumtoa madarakani Rais Francois Bozize ambaye wanamshutumu kuwa hakutimiza ahadi za mkataba wa amani.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.